Sera na Miongozo Kuhusu TEHAMA

Jun 9, 2020

1. SERA YA TEHAMA

Madhumuni ya sera hii ni kuhakikisha kuwa matumizi ya TEHAMA yanachangia katika utendaji bora na kuongeza tija, kukuza utafiti, usalama wa matumizi ya teknolojia ya nyuklia kwa ajili ya maendeleo ya wananchi na Taifa kwa ujumla. Teknolojia ya Habari na Mawasiliano (TEHAMA) ni nyenzo muhimu, ambayo mchango wake ni mkubwa katika kuharakisha kufikiwa kwa malengo ya Tume.  Sera hiyo imejikita katika kukuza matumizi ya TEHAMA katika uzalishaji ili kuongeza tija, TEHAMA inatumika kila mahali na katika utoaji wa huduma za aina yoyote za Tume ikiwemo, utoaji wa vibali, leseni uongozi/utawala (e-Governance) n.k.

2. MUONGOZO WA KULINDA MIFUMO YA TEHAMA

Muongozo huu unatoa maelekezo ya jinsi ya kulinda mifumo ya TEHAMA dhidi ya maafa au uharibifu hivyo kudhibiti athari zinazoweza kupunguza utendaji wa Tume

3. SERA YA USALAMA KATIKA MATUMIZI YA TEHAMA

Sera hii inatoa muongozo wa kuzuia udukuaaji wa mifumo ya mtandao pamoja, vitunza kumbukumbu na vifaa vinavyotumika na Tume katika TEHAMA. Hii ni kulinda taarifa nyeti zisipotee

4. MWONGOZO WA MATUMIZI BORA, SAHIHI, NA SALAMA YA VIFAA NA MIFUMO YA TEKNOLOJIA YA HABARI NA MAWASILIANO (TEHAMA)

 Mwongozo huu unahimiza wafanyakazi wa Tume kufuata maelekezo na utaratibu bora katika matumizi mbalimbali ya TEHAMA na vifaa vinavyohusiana na teknolojia hiyo ikiwemo matumizi ya barua pepe, vitunza kumbukumbu na huduma za mtandao. Aidha, mwongozo unatoa maelekezo na taratibu zinazotakiwa kufuatwa pale inapotokea vifaa vya TEHAMA vinapofanyiwa matengenezo. Mwongozo unatoa Maelekezo kuhusu udhibiti wa maambukizi ya virusi vya kompyuta kwani changamoto kubwa inayoikabili  Serikali sasa ni maambukizo ya virusi vya kompyuta ambayo yanaweza kusababisha  taarifa muhimu na nyeti kupotea au kuvuja.

 

Hifadhi za nyaraka