Dkt. Leonard Akwilapo, Katibu Mkuu Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia Amefanya Ziara, Tume ya Nguvu za Atomiki Tanzania

Dec 1, 2019

Katibu Mkuu, Wizara ya Elimu Sayansi na Teknolojia Dkt. Leonard Akwilapo leo tarehe 30 Novemba, 2019 amefanya ziara Makao Makuu ya Tume ya Nguvu za Atomiki Tanzania Jijini Arusha.

Dkt. Akwilapo alipata ripoti ya Mkurugenzi Mkuu Profesa Lazaro Busagala iliyoahinisha utendaji wa TUME yakiwemo mafanikio mbalimbali ambayo yamefikiwa katika kipindi cha mwaka mmoja na miezi nane tangu alipoteuliwa  na Mhe. Rais kuwa Mkurugenzi Mkuu wa Tume ya Nguvu za Atomiki, kama vile kurejesha maelewano na mahusiano na wafanyakazi kwa njia mbalimbali, kutatua tatizo la upandishwaji madaraja na mishahara tatizo ambalo lilidumu kwa muda mrefu, hati safi ya ukaguzi wa hesabu za Serikali kutoka Ofisi ya Taifa ya Ukaguzi (CAG) kwa mwaka 2017/2018 na 2018/2019, Kuongeza kasi ya utendaji na nidhamu ya watumishi, ufunguzi wa ofisi tisa (9) mpya za mipakani na ikiwemo moja (1) ya kanda ya maziwa makuu ili kusogeza huduma kwa wananchi hivyo kuinua shughuli za kiuchumi, kupunguza muda wa utoaji wa vibali kwa wafanyabiashara, kufanya vikao vya mara kwa mara katika ngazi za vitengo, Idara na Kurugenzi  

Akiongea na Menejimenti Dkt. Akwilapo ameipongeza  TAEC kwa kupata tuzo ya mwajiri bora iliyotolewa na TUCTA kwenye maadhimisho ya meimosi huku akisisitiza kuendelea na vikao mbalimbali ili kutatua matatizo ya wafanyakazi kwa nia ya kuboresha utendaji na kufanya mahala pa kazi kuwa salama

Hifadhi za nyaraka