Idara ya Mabaki ya Mionzi

Kuhusu Idara

Kitengo cha Uhifadhi wa Mabaki ya Vyanzo vya Mionzi kipo chini ya Kurugenzi ya Teknolojia ya Nyuklia na Huduma za Kiufundi (DTTS), ambayo jukumu lake kubwa ni kuhamasisha matumizi salama ya teknolojia ya nyuklia, pamoja na kubainisha fursa ambapo teknolojia ya nyuklia inaweza kutumika kwa ajili maendeleo endelevu.

Kazi za Idara ya Uhifadhi Mabaki ya Vyanzo vya Mionzi

Kitengo cha Uhifadhi wa Mabaki ya Vyanzo vya mionzi kinazo kazi mbalimbali kama zilifuatazo:-

  1. Kukusanya na kusafirisha mabaki ya vyanzo vya mionzi na kuyahifadhi katika Jengo Maalumu la kuhifadhi mabaki hayo (CRWMF)
  2. Kuhifadhi taarifa zote za mabaki ya vyanzo vya mionzi (DSRS) pamoja na vyanzo vya mionzi vinavyotumika (Inventory)
  3. Kuandaa miongozo mbalimbali kwa ajili ya kuboresha masuala ya ulinzi na usalama katika Jengo la kuhifadhi mabaki ya Vyanzo vya mionzi (CRWMF)
  4. Kuandaa utaratibu wa kuomba vibali katika mamlaka ya udhibiti wa matumizi ya vyanzo vya mionzi (Regulator)
  5. Kutafuta na kuviweka  chini ya ungalizi vyanzo vyote vya mionzi vilivyotelekezwa hapa nchini (Orphan Source Search and Secure)
  6. Kufanya uchunguzi na kuimarisha udhibiti wa Jengo la CRWMF (surveillance and Control of CRWMF)
  7. Kufanya ukarabati wa “containers” zinazohifadhi vyanzo vya mionzi ili kupunguza ujazowa “containers”  hizo na hatimae vyanzo vingi vya mionzi kuhifadhiwa katika “containers” moja ndogo.
  8. Kuratibu uandaaji wa sera ya uhifadhi wa mabaki ya vyanzo vya mionzi nchini.
  9. Kuratibu uaandaaji wa mpango wa kitaifa wa kupambana na majanga ya kinyuklia.
  10. Kuandaa program ya kinga ya mionzi katika jengo la CRWMF(Radiation Protection Programme)
  11. Kuandaa mpango wa tathimini ya usalama katika Jengo la CRWMF (safety case and safety assessment)
  12. Kuratibu uandaaji wa miundombinu ya uteketezaji wa mabaki ya vyanzo vya mionzi (final disposal)

Habari na matukio ya Idara

Hakuna Matokeo Iliyopatikana

Ukurasa uliouomba haukuweza kupatikana. Jaribu kusafisha utafutaji wako, au tumia urambazaji hapo juu ili kupata chapisho.

Hifadhi za nyaraka