Idara ya Msaada Wa Kiufundi na Kinga ya Mionzi

Kuhusu Idara

IDARA YA HUDUMA ZA KIUFUNDI NA KINGA YA MIONZI

TAEC ilianzisha idara ya huduma za kiufundi na kinga ya mionzi  ili kuongeza ifaninisi katika shughuli zake za kisheria katika kudhibiti uchafuzi wa mionzi katika mazingira, chakula na mbolea kwa kusudi la kulinda watu na mazingira kutokana na athari mbaya za mionzi. Vipimo anuwai vya silaha za nyuklia na  matukio ya kihistoria kutokana na ajali katika  viwanda vya umeme vya Chernobyl mnamo 1986, na Fukushima Daichii mnamo 2011 na vipimo vingine vingi vinavyoendelea, imelazimu Tume kutekeleza majukumu yake ya kiutendaji katika Maabara zake ili kuhakikisha huduma zake zinakubalika kimataifa ifikapo mwaka 2025.

 Majukumu Ya Idara Ya Huduma Za Ufundi Za Kiufundi Na Kinga Ya Mionzi

·         Upimaji na uchambuzi wa viwango vya mionzi katika sampuli za vyakula na mazingira

·         Upimaji na uchambuzi wa viwango vya mionzi katika mwili wa binanadamu

·         Kufanya Vipimo vya viasili katika sampuli mbalimbali

·         Kufanya tathmini ya athari ya mionzi katika mazingira wakati wa majanga ya kinuklia na kiradiolojia

·         Kutoa huduma za matengenezo na uhakiki wa ubora wa vifaa vya mionzi, maabara, kitabibu na uchunguzi wa magonjwa,

·         Kutoa huduma za upimaji wa mionzi kwa wafanyakazi na uchambuzi wa usalama wa mionzi mahali pa kazi

·         Kusimamia utekelezaji wa majukumu ya kituo cha CTBTO

 MAABARA YA GAMMA- VIPIMO VYA CHAKULA

·         Kupima viwango vya mionzi kwenye vyakula

·         Kupima viwango vya mionzi kwenye mbolea

·         Kupima viwango vya mionzi kwenye tumbaku na sigara

·         Upimaji wa mionzi kwenye sampuli za mazingira zilizochafuliwa kama vile maji, udongo na hewa.

·         Kufanya utafiti juu ya sampuli za mazingira (udongo, maji, mchanga, hewa, chakula na sampuli zozote za mazingira)

·         Uchambuzi wa viwango vya mionzi kwenye sampuli zilizochafuliwa

ALPHA SPECTROSCOPY

·         Upimaji wa udongo na Biota kutambua kiwango cha URANIUM katika Sampuli.

·         Upimaji wa udongo na Biota kutambua kiwango cha POLONIUM katika sampuli

·         Kufanya utaratibu na utafiti juu ya sampuli za mazingira (udongo, maji, mchanga, hewa, chakula na sampuli zote za mazingira.)

 

XRF/TXRF SPECTROSCOPY

o   Kutambua aina ya viasili vilivyopo katika sampuli za kijiolojia na kibaiolojia kwa kutumia kifaa cha XRF na TXRF

o   Kutambua kiasi cha viasili kilichopo katika vyakula

o   Kutambua viasili na kiasi chake katika sampuli za kimazingira

o   Kufanya tafiti mbalimbali zinazouhusiana na sampuli za kimazingira ikiwemo udongo, maji, vyakula, hewa n.k

 HUDUMA ZA MATENGENEZO, NIM

Mikakati ya muda mrefu ya kitengo cha matengenezo ya vifaa vya kieleckronik, umeme na vya nyuklia, NIM ni kuimarisha na kujenga uwezo katika matengenezo ya vifaa tajwa kitaifa.

Baadhi ya Huduma zitolewazo ni:-

Ø  Usimikaji, matengenezo na uhakiki wa vifaa vya mionzi ya nyuklia, vifaa vya maabara pamoja na vifaa vya mionzi vinavyotumika katika tafiti, viwandani na kitabibu. Vifaa au mashine hizi ni kama zifuatavyo: mashine za mionzi ya X-Rays, CT scan, Ultrasound, mashine tiba za saratani, mashine za kutambua na kupima mionzi.

Ø  Uhakiki na marekebisho ya vifaa vinavyotumia teknolojia ya mionzi kupimia unyevunyevu na mgandamizo wa udongo (mashine za Troxiler na Humboldt).

Ø  Kuunda na kutengeneza vifaa vya gharama ndogo vya kielektroniki kwa matumizi ya kawaida.

Ø  Kutoa na kusimamia mafunzo kuhusu vifaa vya nyuklia kwa Wahandisi na mafundi mchundo katika maeneo mbalimbali hasa viwandani, migodini, Hospitalini, na utafiti wa kisayansi.

Ø  Kutoa huduma ya ushauri wa kiufundi na manunuzi kwa vifaa vya kisayansi, kitabibu na vifaa vya kielektroniki.

Ø  Kuhamasisha wanafunzi kutoka vyuo mbalimbali katika kuendeleza technolojia hii ya vifaa vya nyuklia wakati wa mafunzo kwa vitendo.

 MAABARA YA KUPIMA VIWANGO VYA MIONZI KWA WAFANYAKAZI

Kuapo kwa mionzi katika eneo la kazi inatokana na uwepo wa nje wa mionzi unaotokana na viasilia vya mionzi vinavyosababishwa na matukio mbalimbali ya matumizi ya mionzi.

Hii inatokana na kazi zinazohusiana na hatua mbalimbalii katika uchakataji wa nuklia, utumiaji wa vyanzo vya mionzi katika matumizi ya matibabu, tafiti za kisayansi, Kilimo, Viwanda na hata katika urutubishaji wa Urani.

Upimaji wa viwango vya mionzi kwa wafanyakazi katika vyanzo vya mionzi Tanzania ulianza mnamo mwaka 1986 na maabara mpaka sasa ina uwezo wa kupima wafanyakazi 2000 wanao fanyakazi katika vyanzo vya mionzi. Hii Huduma ni ya kisheria katika leseni za uendeshaji shughuli kwa kutumia vyanzo vya mionzi.

HUDUMA ZETU

a.      Kuhakikisha Utumiaji mzuri wa vyanzo vya mionzi kwa mfanyakazi katika mazingira ya kazi.

b.      Kutoa Viwango vya mionzi walivyopata wafanyakazi wanaofanya kazi katika maeneo ya mionzi na wamekithi matakwa ya kisheria

c.       Kutoa utaratibu mzuri wa jinsi ya kufanya kazi katika eneo ambalo kuna mionzi na kuhakikisha utendaji kazi ni mzuri na hauadhiri afya ya mfanyakazi

d.      Kutoa taarifa zitakazoweza kumsaidia mfanyakazi anayefanya kazi katika vyanzo vya mionzi wa lengo la kupunguza kupata mionzi mingi eneo la kazi

e.      provision of information for the evaluation of dose in the event of accidental exposures

Kutoa taarifa na uchambuzi wa mionzi endapo kukatokea ajali ya mionzi katika eneo lenye vyanzo vya mionzi

Pia, Viwango vya mionzi tunavyopima vinatusaidia katika

i.            .Katika upimaji wa athari za mionzi

ii.            Kuhifadhi data za mionzi zinazosaidia tafiti mbalimbali

iii.            Upimaji wa viwango vya mionzi kwenye mazingira

 MAABARA YA TAIFA YA UHAKIKI WA VIFAA VYA MIONZI

.Kuanzishwa kwa Maabara

TAEC ilianzisha maabara ya taifa ya daraja la pili la viwango vya mionzi ayonishi mnamo mwaka 1991 ikijulikana kama NRC. Miaka baadaye ilijiunga na uanachama wa Shirika la nguvu za Atomu Duniani ikishirikiana na Shirika la Afya Duniani katika Umoja Huo wa Kimataifa. Nchi za jirani zimeonyesha ushirikiano kwa uwapo wa maabara hii katika kuhakikisha Inatoa huduma ya uhakiki wa vifaa vya mionzi ndani na Nje ya Nchi.

Huduma Zetu

Maabara ya daraja la pili ya viwango vya mionzi vinatoa huduma ya uhakiki wa vifaa vinavyopima mionzi ayonishi  na pia inatoa Vyeti vya Uhakiki. Maabara ya Uhakiki wa Vifaa vya mionzi tunatumia vizio kama Gray, Sievert (Sv) na Becquerel

 

Eneo Kazi
Tiba kansa Uhakiki wa vifaa vya mionzi na Kushirki katika ushiriki wa uwiano wa tiba kansa na maabara nyingine duniani katika mashine ya Kobalt 60 katika tiba kansa
Eksirei Uhakiki wa vifaa vya mionzi katika Idara za Eksirei
Kinga Mionzi Uhakiki wa vifaa vya mionzi na Uhakiki wa Vipima mionzi vya wafanyakazi

Maabara Pia inashiriki katika mazoezi mbalimbali ya mwingiliano na nchi za maabara nyingine kujihakikishia huduma tunayotoa inafuata taratibu zilizowekwa za kimataifa.

 

Habari na matukio ya Idara

Hakuna Matokeo Iliyopatikana

Ukurasa uliouomba haukuweza kupatikana. Jaribu kusafisha utafutaji wako, au tumia urambazaji hapo juu ili kupata chapisho.

Hifadhi za nyaraka