Idara ya Utawala na Rasilimali Watu
Kuhusu Idara
Sekshieni hii inahusika katika kusimamia miongozo yute ya Serikali inayohusiana na masuala ya rasilimali watu kama vile sheria, kanuni,sera pamoja namiongozo mingine inayoongoza Utumishi wa Umma. Pia, kinaongoza na kusimamia masuala yote yanayohusu utawala na utumishi wa Tume. Zifuatzao ni shughuli/majukumu ambazo/yo hufanywa na seksheni hii:
- Kutafsiri na kutekeleza Sheria ya Utumishi wa Umma ya mwaka 2002 na kanuni zake za mwaka 2003, Kanuni za Kudumu za Utumishi wa Umma za mwaka 2009, Sheria ya Tume ya Nguvu za Atomiki ya mwaka 2003 na Kanuni yake ya mwaka 2017, Sheria ya Ajira na mahusiano kazini ya mwaka 2004 na kanuni zake za mwaka 2007 na Sheria, Kanuni, Nyaraka na Miongozo mbalimbali inayohusu masuala ya Utumishi wa Umma.
- Kushughulikia upatikanaji, ukuzi, upangaji kazi, uthibitisho, upandaji vyeo, Uhamisho na uachishaji kazi Rasilimali Watu.
- Kusaidia katika maandalizi ya bajeti ya mishahara na marupurupu mengine ya Rasilimali Watu
- Kusaidia katika menejimenti ya Rasilimali Watu, uhusiano wa kazini pamoja na nidhamu ya wafanyakazi.
- Kusaidia katika kupanga mafunzo na maendeleo ya wafanyakazi pamoja na kupanga programme za kuendeleza Rasilimali Watu.
- Kusaidia katika kuandaa, kuchambua mifumo ya kazi, marupurupu na kanuni za kazi.
- Kushiriki katika kuandaa sera zaUtawala kuhusiana na kazi zaTume.
- Kuongoza katika utekelezaji wa sera zinazohusu masuala ya jinsia, usalama, ulemavu, HIV/AIDS na afya kwa ujumla.
- Kukusanya, kuchambua na kutunza kumbukumbu za Rasilimali Watu pamoja na Takwimu muhimu.
HALI YA UTUMISHI
Mpaka kufikai Aprili 2019, Tume inajumla ya watumishi 114 ambao wana ajira za kudumu na wanatumikia katika ofisi mbalimbali za Tume nchini. Kati ya watumishi 114, watumishi 81 ni wanaume na watumishi 33 ni wa kike.
MAFUNZO NA SEMINA KWA WATUMISHI
Seksheni inaandaa mafunzo na semina mbalimbali kwa watumishi wake kuhusuana na masuala mtambuka kama Ukimwi na Virusi vya Ukimwi, Magonjwa yasiyo ya kuambukiza, Kupambana na kuzuia rushwa pahala pa kazi, Utawala Bora, kupitia wataalamu kutoka Ofisi ya Rais, Mejementi ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Hospitali za Umma pamoja na Taassis mahsusi za Umma kwa ajili ya kutoa mafunzo.
Habari na matukio ya Idara
Hakuna Matokeo Iliyopatikana
Ukurasa uliouomba haukuweza kupatikana. Jaribu kusafisha utafutaji wako, au tumia urambazaji hapo juu ili kupata chapisho.