Kitengo cha Udhibiti

Kuhusu Kitengo

Kazi ya Udhibiti:

  1. Kuanzisha na kutekeleza au kutekeleza mfumo wa udhibiti na uidhinishaji kupitia usajili na utoaji leseni za uingizaji, usafirishaji, usambazaji, umilki na utumiaji wa vyanzo vya mionzi;
  2. Kupitia maombi ya matumizi salama ya mionzi kutoka kwa wadau wote kabla ya kuidhinishwa na kufanya hivyo baada ya muda maalum, wakati wa matumizi kama inavyotakiwa;
  3. Kufanya ukaguzi na kuhakikisha kuwa hatua za marekebisho zitachukuliwa kama itabainika  hali isiyo salama au inayoweza kuleta madhara;
  4. Kufanya udhibiti wa kisheria juu ya mambo yote yanayohusiana na mionzi ayonisha na mionzi isiyoayonisha;
  5.  Kuanzisha na kufanya kazi au kuwezesha uanzishaji na operesheni ya mfumo wa udhibiti wa athari za viasilia vya mionzi katika vyakula, malisho ya wanyama na mazingira; pamoja na usimamizi wa mabaki ya mionzi yanayotokana na matumizi anuwai ya Nguvu ya atomiki na teknolojia ya nyuklia;
  6. Kuunda, kuendesha na kutekeleza mpango wa kitaifa wa dharura wa kukabiliana na majanga ya kiradiolojia na utayari;
  7.  Kuchunguza shughuli zote zinazohusu, mionzi au eneo la mionzi na pale ambapo kuna uvunjaji wa viwango vya usalama, kuagiza kufungwa au kuchukua hatua ya kufunga shughuli hiyo au majengo hayo.

 

Soma zaidi Kuhusu Huduma Zinazotelewa na Tume

Habari na matukio ya Kitengo

Hakuna Matokeo Iliyopatikana

Ukurasa uliouomba haukuweza kupatikana. Jaribu kusafisha utafutaji wako, au tumia urambazaji hapo juu ili kupata chapisho.

Hifadhi za nyaraka