KUHUSU TUME YA NGUVU ZA ATOMIKI TANZANIA (TAEC)

Tume ya Nguvu za Atomiki Tanzania (TAEC) ilianzishwa kwa Sheria ya Bunge Na.7 yamwaka 2003 (The Atomic Energy Act. No.7 of 2003). Awali ilikuwa ikijulikana kama Tume ya Taifa ya Mionzi (National Radiation Commission) iliyoanzishwa kwa Sheria ya Bunge Na.5 ya mwaka 1983 (The Protection from Radiation Act. No.5 of 1983)

Majukumu ya Tume

a) Kudhibiti matumizi salama ya mionzi nchini.

b) Kuhamasisha na kuendeleza matumizi salama ya teknolojia ya nyuklia

c) Kufanya utafiti na kutoa ushauri na taarifa mbalimbali juu ya sayansi na teknolojia ya nyuklia

Kazi za TAEC

  1. Kukagua vituo vyote vyenye vyanzo vya mionzi ili kusimamia utekelezaji wa sheria ya Nguvu za Atomiki na kanuni zake
  2. Kutoa vibali vya uingizaji, umiliki, usafirishaji na utumiaji wa vyanzo vya mionzi.
  3. Kupima sampuli za vyakula, mbolea, vyakula vya wanyama, tumbaku na mazao yake vinavyoingizwa na kusafirishwa nje ya nchi.
  4. Kupima sampuli za mazingira ili kubaini uchafuzi wa mionzi kwenye mazingira.
  5. Kupima kiwango cha mionzi kwenye minara ya simu na rada za mawasiliano.
  6. Kukusanya, kusafirisha na kuhifadhi mabaki vyanzo vya mionzi.
  7. Kutoa huduma ya upimaji wa mionzi kwa wafanyakazi wanaofanyakazi kwenye maeneo yenye vifaa vya mionzi.
  8. Kuendesha kituo cha kupima uchafuzi wa anga (air pollution) unaotokana na majaribio ya silaha za nyuklia (Radionuclides Monitoring Station- RN64).
  9. Kuratibu miradi mbalimbali ya matumizi ya teknolojia ya nyuklia hapa nchini.
  10. Kutoa elimu kwa umma juu ya faida na madhara ya teknolojia ya nyuklia
  11. Kuendeleza tafiti za teknolojia ya nyuklia kwa maendeleo endelevu ya kiuchumi na kijamii.

Kutoa huduma za matengenezo ya vifaa vinavyotumia teknolojia ya nyuklia kama vile X-Ray, CT-Scan, na MRI n.

TAEC Headquarters-Arusha

Tume ya Nguvu za Atomiki Tanzania (TAEC) ni taasisi maalum ya Serikali inayohusika na masuala yote ya nishati ya atomiki katika Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

DIRA

“Kuwa kituo bora katika kudhibiti na kuhamasisha matumizi salama ya Teknolojia ya nyuklia Afrika”

 

DHIMA

“Kukuza matumizi salama na ya amani ya sayansi ya nyuklia na teknolojia kwa maendeleo endelevu ya kiuchumi na kudhibiti matumizi ya teknolojia ya nyuklia ili kulinda umma, wafanyikazi na mazingira kutokana na athari mbaya ya mionzi”

MUUNDO WA TUME

WAJUMBE WA BODI YA  TUME