Mafunzo ya Kitaifa ya Usalama wa Mionzi kwa Wataalam Wanaotumia Vyanzo vya Mionzi kwenye Ukaguzi wa Mizigo na Tiba, 20-24 Septemba 2021, Arusha

Sep 21, 2021

Wataalam  wanaotumia vyanzo vya mionzi kwa ajili ya ukaguzi wa mizigo bandalini, utafiti na matibabu ya magojwa mbalimbali wanashiriki katika mafunzo ya Kitaifa ya Usalama wa Mionzi yanayoendeshwa na Tume ya Nguvu za Atomu Tanzania (TAEC) jijini Arusha.

 Mafunzo haya yanafanyika kwa muda wa siku tano, ambapo kilele chake ni siku ya Ijumaa tarehe 24 Septemba 2021.

Jumla ya Wataalamu 27 wanashiriki mafunzo haya ambapo wataalamu 18 kutoka mamlaka ya bandari Tanzania (TPA), Hospitali ya Rufaa ya Bugando washiriki 3, Taasisi ya Saratani ya Ocean Road mshiriki 1, Hospitali ya Agha Khan ya Jijini Dar es Salaam mshirki 1, Hospitali ya Benjamini Mkapa ya Jijini Dodoma mshiriki 1 na Shirika la viwango Tanzania (TBS) washiriki 3

Lengo kuu la mafunzo haya ni kuwezesha wataalamu wanaotumia vyanzo vya mionzi waweze kujua mbinu bora ya kujikinga na madhara yanayoweza kusababishwa na mionzi,  ili kulinda wafanyakazi, wananchi, wagonjwa na mazingira.

Vilevile wataalamu hawa waweze kutambua  viwango vya mionzi ambavyo ni salama kwa wananchi na wafanyakazi  katika maeneo ya kazi ili kuepuka athari zinazoweza kusababishwa na mionzi, hii ni pamoja na kufuata sheria za usalama wa mionzi mahala pa kazi bila kusahau kuzingatia miongozo ya kitaifa na kimataifa inayoelekeza namna salama ya matumizi ya mionzi.

Akifungua mafunzo hayo, kwa niaba ya Mkurugenzi Mkuu wa TAEC, Mkurugenzi wa Kitengo cha Udhibiti wa Mionzi, TAEC, Dkt. Justine Ngaile amewataka washiriki hao kuhakikisha wanapata uelewa mzuri katika mafunzo hayo ili kuhakikisha wanajikinga na  kuwakinga wananchi dhidi ya madhara yatokanayo na mionzi.

Hifadhi za nyaraka