Taarifa kwa wadau na wateja kuhusu mfumo wa malipo – ‘GePG’

Jun 19, 2018

TUME YA NGUVU ZA ATOMIKI TANZANIA

TAARIFA KWA UMMA
KUFANYA MALIPO KUPITIA MFUMO MPYA WA SERIKALI WA (GePG)

Tume ya Nguvu za Atomiki Tanzania (TAEC) inapenda kuwataarifu wadau na wateja wake wote kuwa kuanzia tarehe 4/4/2018 malipo yote yamekuwa yakifanywa kupitia mfumo wa malipo wa Serikali, “Government Electronic Payment Gateway” (GePG) Hivyo basi malipo ya huduma zote zinazotolewa na Tume yalipiwe kupitia mfumo huu ili kukidhi matakwa ya Kisheria ya Serikali na si vinginevyo. Malipo yafanyike kupitia Benki ya NMB na mitandao ya kifedha ya M- Pesa, Tigo-Pesa na Airtel Money. Namba ya Kampuni ni 888999 na Namba ya Kumbukumbu (Control Number) itapatikana baada ya kuwasiliana na Tume na kupewa hati ya madai (Government Bill). Malipo yatakayokiuka utaratibu huu hayatapokelewa.

Epuka usumbufu lipa kwa kutumia mfumo wa GePG.

“Teknolojia ya Nyuklia kwa Maendeleo ya Taifa”

Imetolewa na:

MKURUGENZI MKUU

Hifadhi za nyaraka