Tume ya Nguvu za Atomiki Tanzania (TAEC) na jeshi la Polisi wamesaini makubaliano ya kuongeza ushirikiano wa ulinzi na usalama wa vyanzo vya mionzi pamoja na mambo mengine mbalimbali ikiwemo kuweka ulinzi wakati wa usafirishaji wa vyanzo vya mionzi pamoja na kuhakikisha ulinzi wa vituo vinavyofungiwa kutumia vyanzo vya mionzi kutokana na sababu za ukiukwaji wa sheria na taratibu vinabaki vimefungwa hadi pale vitakapo kidhi masharti na sheria za matumizi salama ya mionzi .
Lengo kuu la makubaliano haya ni kuimarisha zaidi ulinzi na usalama wa vyanzo vya mionzi nchini na kuepusha vyanzo hivyo kuangukia kwenye mikono isiyo salama na kuvitumia vibaya katika matukio ya kihalifu/kigaidi na kuleta taharuki katika jamii
Makubaliano haya yametiwa saini na Kamishna wa Operesheni na Mafunzo wa Jeshi la Polisi Ndugu Liberatus Sabas kwa niaba ya Inspekta Jenerali wa Jeshi la Polisi (IGP), na Profesa Lazaro Busagala, Mkurugenzi Mkuu wa Tume ya Nguvu za Atomiki Tanzania.