Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia inatekeleza mpango wa kukuza fani za Sayansi, Teknolojia, Ubunifu, Uhandisi, Hisabati na Tiba kupitia programu ya Ufadhili wa Samia (Samia Scholarship Extended Program).
Wizara kupitia Tume ya Nguvu za Atomu Tanzania (TAEC) inawatangazia Watanzania wenye Sifa kuomba ufadhili wa masomo ya Shahada za Juu (Uzamili) kwa wahitimu wenye ufaulu wa juu zaidi kwenye masomo ya sayansi kutoka katika vyuo vikuu vya Tanzania.
Kwa maelezo zaidi bofya HAPA
Kutuma maombi yako tembelea: samiascholarship.taec.go.tz