Tume ya Nguvu za Atomiki Tanzania (TAEC) imetoa elimu juu ya umuhimu wa upimaji wa mionzi katika zao la kahawa kwa wafanyabiashara wa zao hilo kwenye soko la mnada uliofanyika wilaya ya Moshi Mkoani Kilimanjaro jana tarehe 21/11/2019.
Mnada huo umewashirikisha wafanyabiashara mbali mbali wanaosafirisha kahawa ndani na nje ya nchi ambapo wameweza kupata uelewa wa sababu za upimaji wa mionzi kwenye kahawa na utaratibu mzima wa upatikanaji wa vibali vya kusafirisha zao hilo nje ya nchi bila kutumia mawakala .
Tume amewambia wafanyabiashara hao kuwa lengo la kuhakikisha Tanzania inaendelea kubakia katika soko la kahawa yenye ubora na isiyo na vimelea vya uchafuzi wa mionzi.
“Tume imeeleza sababu za kupima mionzi kwenye kahawa pamoja na wajibu wa kuhakikisha madhara yatokanayo na mionzi hayatokei.
Sheria Na. 7 ya mwaka 2003 ya Nguvu za Atomiki Tanzania imeipa mamlaka TAEC kudhibiti matumizi salama ya mionzi hapa nchini.
TAEC itaendelea kutoa elimu kwa wafanyabiashara mbali mbali nchini juu ya kazi zake kwa lengo la kusaidia kutoa uelewa zaidi juu ya upimaji wa mionzi kwenye bidhaa mbali mbali zinazosafirishwa ndani na nje ya nchi