Wafanyabiashara Wadogo wa Bagamoyo Wapewa Mafunzo ya Utambuzi wa Vifaa vya Mionzi

Jun 30, 2020

WAFANYABIASHARA wadogo wa bandari ya Bagamoyo mkoani Pwani, wamepata elimu ya utambuzi wa bidhaa na vifaa vyenye mionzi ikiwa ni hatua za kuwaelimisha ili watambue madhara ya mionzi na wajue jinsi ya kujikinga.

Hayo yamesemwa na Kaimu Mkuu wa Kanda ya Mashariki wa Tume ya Nguvu za Atomiki Tanzania (TAEC), Alex Muhulo kwenye semina ya siku moja iliyofanyika Wilaya ya Bagamoyo kwa ajili ya wafanyabiasara wadogo wa naotumia bandari hiyo.

Alisema TAEC imerahisisha huduma kwa wafanyabiashara wadogo wanaoingiza bidhaa nchini, kwa kufungua ofisi katika maeneo ya mipakani na bandarini  na kupima sampuli za bidhaa husika kisha kutoa majibu ndani ya muda mfupi hivyo kuokoa muda wa mfanyabiasha huyo.

Akizungumzia maboresho ya utendajikazi wa TAEC na mfumo wa utoaji huduma kwa njia ya mtandao hususan kwa wafanyabiashara wadogo, Muhulo alisema hadi sasa tume hiyo imeshafungua ofisi 24 kwenye mipaka mbalimbali nchini ili kurahisisha utoaji wa huduma kwa kundi la wafanyabiashara hao wasio na uwezo wa kufuata huduma hiyo kwenye ofisi za Kanda au makao makuu.

Alex amewataka wafanyabiashara hao kutambua kwamba bidhaa zina mionzi hivyo ni vyema wakafuata taratibu za kisheria za uingizaji wake kutoka nje ili ziwe salama na zisilete madhara kwao na kwa watumiaji wa mwisho.

Kuhusu kuboresha mfumo wa utoaji huduma za TAEC mtandaoni, Muhulo alisema  tume hiyo imejipanga  kuhakikisha wafanyabiashara wanapata huduma kwa muda mfupi ili kusiwe na kikwazo cha utoaji bidhaa zao bandarini na kusababisha hasara.

Kwa sasa wafanyabiashara wadogowadogo wanaoingiza bidhaa zao nchini kupitia bandari mbalimbali wanapata huduma bandarini hapo na pia sampuli huchukuliwa na majibu kurudishwa muda mpufi ya kutambua kiwango cha mionzi kilichopo ikiwa  hatua ya udhibiti wa uingizaji wa bidhaa  hatari kwa binadamu, viumbe hai wengine na mazingira.

Kwa upande wake, Mkuu wa Wilaya ya Bagamoyo, Zainabu Kawawa ambaye alikuw amgeni rasmi katika mafunzo hayo alisema mafunzo hayo yatawasaidia wafanyabiashara hao kuwa na elimu ya mionzi na kutambua jinsi ya kujikinga.

Hifadhi za nyaraka