Wananchi wamepatiwa elimu ya matumizi salama ya mionzi kwenye maonesho ya nanenane mwaka 2020

Aug 14, 2020

Zaidi ya  wananchi 1000 wamepata elimu ya majukumu  ya kisheria Tume ya Nguvu za Atomiki Tanzania (TAEC) na namna ya matumizi salama ya teknolojia ya nyuklia inavyotumika nchini kwenye maonesho ya kitaifa ya Kilimo, Mifugo na Uvuvi ya NaneNane yaliyofanyika katika viwanja vya Kizimbani Zanzibar, viwanja vya Themi Arusha na kitaifa katika viwanja vya Nyakabindi, Wilaya ya Bariadi, Mkoani Simiyu .

Wananchi wameweza kufahamu masuala mbali hasa namna teknolojia ya Nyuklia inavyotumika katika sekta za maji,kilimo,viwanda,madini na afya.

Maonesho  hayo yalifunguliwa rasmi tarehe 01/08/2020 na Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mama Samia Suluhu Hassan na maonesho hayo kufungwa na Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe.Kassim Majaliwa.

Viongozi mbali mbali wa serikali waliotembelea katika maonesho hayo ni pamoja na Naibu waziri wa Mifugo na Uvuvi, Mhe.Abdallah Ulega, wakuu wa mikoa ya Arusha Mhe.Iddi Kimanta, Mkuu wa mkoa wa Kilimanjaro Mhe.Anna Mgwira na Mkuu wa Mkoa wa Simiyu Mhe.Athony Mtaka.

Wengine ni wakuu wa wilaya  ambao ni Mkuu wa Wilaya Arusha Mjini Mhe. Kenani Kihongosi, Mkuu wa Wilaya ya Mwanga  Mhe.Tom Apson.

Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano Peter Ngamilo ameeleza kuwa baadhi ya wananchi waliotembelea katika maonesho hayo wametoa ushauri KWA TAEC kuendelea  kuongeza wigo katika huduma za udhibiti  kwenye maeneo ambayo sio rasmi kama vile katika bandari bubu na maeneo mengine ambayo sio rasmi lakini bidhaa hupitishwa huko kinyemela ili kuweza kudhibiti na kuhakikisha kuwa bidhaa zote zinakaguliwa.

Hifadhi za nyaraka