Waziri Mkuu Azindua Maabara ya Tume ya Nguvu za Atomiki Tanzania

May 3, 2019

Waziri  Mkuu wa Jamhuri ya muungano wa Tanzania Mhe. Kassim Majaliwa amezindua Maabara ya kisasa ya Tume ya Nguvu za Atomiki Tanzania na kufungua mkutano wa Pili wa Pamoja wa Mtandao wa Vyombo vya Udhibiti wa Nyuklia kwa Jumuiya ya Maendeleo ya Nchi za Kusini mwa Afrika (SADC)   Aprili 29, 2019

Picha kushoto inamuonyesha Waziri  Mkuu Kassim Majaliwa, akioneshwa kifaa cha kupimia mionzi na Mkurugenzi wa Kinga ya Mionzi, Dkt Firm Banzi, baada ya kuzindua Maabara ya Tume ya Nguvu za Atomiki Tanzania Aprili 29, 2019.

Picha kulia inamuonyesha Waziri  Mkuu Kassim Majaliwa, akizungumza, katika mkutano wa Pili wa Pamoja wa Mtandao wa Vyombo vya Udhibiti wa Nyuklia kwa Jumuiya ya Maendeleo ya Nchi za Kusini mwa Afrika (SADC) Aprili 29, 2019.

Picha kushoto inamuonyesha Waziri  Mkuu Kassim Majaliwa, akisalimiana na Meneja Muandamizi wa Kituo cha Kimataifa cha Sayansi na Teknolojia na Mshauri wa Masuala ya Kidiplomasia (ISTC), Dkt. Kamen Velichkov, baada ya kufungua mkutano wa Pili wa Pamoja wa Mtandao wa Vyombo vya Udhibiti wa Nyuklia kwa Jumuiya ya Maendeleo ya Nchi za Kusini mwa Afrika (SADC) Aprili 29, 2019.

Hifadhi za nyaraka