Waziri wa Elimu Sayansi na Teknolojia Prof. Adolf Mkenda amekutana na kufanya mazungumzo na Mkurugenzi Mkuu wa TAEC

Jul 12, 2024

Waziri wa Elimu Sayansi na Teknolojia Prof. Adolf Mkenda amekutana na kufanya mazungumzo na Mkurugenzi Mkuu wa Tume ya Nguvu za Atomu Tanzania (TAEC), Prof. Najat Kassim Mohammed ofisi za wizara jijini Dodoma.

Mazungumzo hayo yamefanyika kwa mara ya kwanza tangu Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan alipomteua Prof. Najat kuwa Mkurugenzi Mkuu wa TAEC.

TAEC ni taasisi inayohusika na udhibiti wa matumizi salama ya mionzi nchini na uhamasishaji wa matumizi salama ya  teknolojia ya nyuklia nchini ambapo Taasisi hii ipo chini ya Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia.

“Mionzi kwa Matumizi Salama na Teknolojia ya Nyuklia kwa Maendeleo ya Taifa”

Hifadhi za nyaraka