Wito kwa makampuni, Taasisi na watafiti kutembelea Tume kujifunza juu ya mionzi isiyoayonissha

Dec 3, 2019

Taasisi, Watafiti na makampuni mbali mbali hapa nchini yanayohusika na vyanzo vya mionzi isiyo ayonisha (Non Inonizing Radiation) kama vile makampuni ya simu (Base Tranasceiver stations),watumiaji wa vifaa tiba (MRI & Utra sound) wametakiwa kutembelea Makao Makuu ya Tume ya Nguvu za Atomiki Tanzania (TAEC) kwa lengo la kujifunza na kupata kupata ujuzi utakaosaidia kulinda usalama wa wafanyakazi mahala pa kazi, wananchi na mazingira dhidi ya madhara yanayoweza kusababishwa na mionzi isiyoayonisha.

Hayo yamesemwa na Afisa Mtafiti wa vifaa vya Nyuklia, katika Idara ya Mionzi isiyo Ayonisha Injinia. Christina Nyakyi katika mahojiano maalumu ambapo amesema kwa kufanya hivyo kutasaidia sana kuboresha ulinzi na usalama mahala pa kazi kwa wafanyakazi, wananchi na mazingira kuhusiana na mionzi ya aina hiyo hapa nchini.

“Tunatoa wito wa watafiti na makampuni kuja kupata ujuzi utakaowasaidia kujilinda ili kuwa salama katika maeneo yao ya kazi kwa lengo la kulinda binadamu na mazingira” alisema Bi Christina.

Bi. Christina., amesema kuwa Sheria namba 7 ya mwaka 2003 ya Tume ya Nguvu za Atomiki Tanzania(TAEC) sehemu ya 7 kifungu namba 48-50, inatoa mamlaka ya kusimamia na kukagua maeneo mbali mbali yenye mionzi isiyo ayonisha kama vile kwenye minara ya simu, vituo vya Usambazaji wa Masafa ya utangazaji, vituo vya rada, katika laini kubwa za usambazaji wa umeme pamoja na vifaa tiba vyenye asili hiyo.

Amesema pia Tanzania iko chini ya Tume ya Kimataifa ya Udhibiti wa Mionzi isiyo ayonisha ICNIRP (International Commission on Non-Ionizing Radiation Protection) inawataka kufanya ukaguzi wa mara kwa mara kwa watoa huduma za namna hiyo ili kujiridhisha wote wenye kutumia vifaa hivyo nchini kama wanakidhi vigezo husika.

Tume ya Nguvu za Atomiki Tanzania (TAEC) ilianzishwa kwa sheria ya Bunge namba 7 ya mwaka 2003 ambapo dhima yake kusimamia na kudhibiti matumizi salama ya mionzi ili kulinda umma,wafanyakazi pamoja na mazingira dhidi ya madhara ya mionzi na kuhamasisha matumizi salama ya teknolojia ya nyuklia kwa kwa maendeleo endelevu ya kijamii na kiuchumi.

Hifadhi za nyaraka