DR. ROBERT FLOYD AIPONGEZA TUME YA NGUVU ZA ATOMU TANZANIA (TAEC)
Published on July 02, 2025

Katibu Mtendaji wa Mkataba wa kupiga marufuku majaribio ya silaha za nyuklia (CTBTO) Dkt. Robert Floyd ameipongeza Tume ya Nguvu za Atomu Tanzania (TAEC) kwa namna inavyosimamia vyema kituo cha kupima uchafuzi wa anga kutokana na matumizi ya teknolojia ya nyuklia.
Dkt. Floyd ameyasema hayo jijini Dar es salaam katika mhadhara uliofanyika katika chuo kikuu cha Dar es salaam ukibeba ajenda ya namna ya kuendeleza mafanikio ya mkataba wa kupiga marufuku majaribio ya silaha za nyuklia (CTBTO).
Dkt. Floyd amesisitiza kuwa Tanzania inapaswa kujivunia kwa kuwa na kituo ambacho kinaisaidia dunia kufahamu hali ya usalama na ofisi yake itaendelea kutoa mafunzo kwa wataalamu wa kitanzania ili kujiimarisha zaidia katika eneo hilo.
Kwa upande wake Mkurugenzi Mkuu wa Tume ya Nguvu za Atomu Tanzania Prof. Najat Kassim Mohammed amesema majaribio ya silaza za nyuklia yanapingwa dunia nzima hivyo Tanzania kuwa na kituo cha kupima uchafuzi wa anga ni njia bora ya kujiridhisha kwamba hakuna uchafuzi utokanao na majaribio ya matumizi ya silaha za nyuklia na ukitokea nchi iweze kuwa na taarifa.