Dira na Dhima
Published on January 20, 2025
Dira
TAEC ina maono ya kuwa “taasisi ya kiwango cha kimataifa katika kudhibiti na kuendeleza matumizi ya amani na usalama ya sayansi na teknolojia ya nyuklia”
Dhamira
Dhamira ya Tume ni “Kudhibiti na kuendeleza matumizi ya sayansi na teknolojia ya nyuklia kwa njia ya amani na salama kwa maendeleo endelevu ya kijamii na kiuchumi.”
Maadili ya Msingi:
1. Uwajibikaji: Wafanyakazi wa TAEC wanawajibika kwa maamuzi na vitendo vyao;
2. Uadilifu: Wafanyakazi wa TAEC hutumia viwango vya juu vya maadili vinavyoonyesha uaminifu na haki katika kila hatua wanayochukua;
3. Ubunifu: Uongozi wa TAEC unahamasisha ubunifu, mawazo mapya na kutambua michango inayoboresha utendaji kazi;
4. Kushirikiana: Wafanyakazi wa TAEC hufanya kazi kwa pamoja, kubadilishana uzoefu na kuheshimiana ili kufanikisha lengo la pamoja;
5. Ujibu wa haraka: Wafanyakazi wa TAEC hutoa majibu kwa wakati muafaka na kwa njia inayofaa kulingana na mahitaji ya wadau;
6. Uwazi: Wafanyakazi wa TAEC huendesha shughuli za Tume kwa uwazi wa hali ya juu.