Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Tume ya Nguvu za Atomu Tanzania

"Mionzi kwa Matumizi Salama na Teknolojia ya Nyuklia kwa Maendeleo ya Taifa"
Nyumbani / Habari / SERIKALI YAWEKEZA KATIKA HOSPITALI NNE ZA SARATANI KUPUNGUZA CHANGAMOTO ZA MATIBABU NCHINI.

SERIKALI YAWEKEZA KATIKA HOSPITALI NNE ZA SARATANI KUPUNGUZA CHANGAMOTO ZA MATIBABU NCHINI.

SERIKALI YAWEKEZA KATIKA HOSPITALI NNE ZA SARATANI KUPUNGUZA CHANGAMOTO ZA MATIBABU NCHINI.

Published on February 06, 2026

Article cover image

Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Mhe. Hemed Suleiman Abdullah amesema serikali inaendelea na uwekezaji wa hosipitali nne za kutibu saratani nchini ili kupunguza changamoto ya matibabau ya saratani kwa wananchi ambao hutegemea hosipitali za serikali za Ocean Road na Bugando kupata matibabu.

Akizungumza wakati wa ufunguzi wa mkutano unaozungumzia mradi wa kupambana na saratani katika nchi wanachama wa Shirika la Nguvu za Atomu Duniani (IAEA) upande wa Afrika (RAF 6060) Mhe. Hemed amesema Tanzania inaendela na mkakati wa kuhakikisha Hospitali ya Rufaa ya KCMC, Hospitali ya Rufaa ya Benjamin Mkapa Jijini Dodoma, Hospitali ya Rufaa ya Mbeya na Hospitali ya Mnazi mmoja Zanzibar zinaanza kutoa huduma ya matibabu ya saratani ili kusogeza huduma karibu na wananchi.

Kwa upande wake Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Zanzibar ambaye pia ni Kaimu Waziri wa Afya Mhe.  Dkt. Saada Mkuya amesema Zanzibar inatarajia kuanza ujenzi wa Taasisi ya Saratani mapema mwaka huu jambo ambalo litawaondolea wakazi wa Zanzibar adha ya kufuata matibabu ya saratani Ocean Road Jijini Dar es salaam.

Akimwakilisha Mkurugenzi Mkuu wa Tume ya Nguvu za Atomu Tanzania, Mkurugenzi wa Kinga ya Mionzi TAEC Dkt. Justin Ngaile amesema mradi wa RAF 6060 ni mradi wa miaka minne ambao umelenga kuzisaidia nchi za Afrika ambazo ni wanachama wa Shirika la Nguvu za Atomu Duniani (IAEA) kukabiliana na ongezeeko la ugonjwa wa saratani ambapo mkutano wa nchi wanachama utasaidia kubadilishana uzoefu na kuwa na maazimio ya pamoja ya kuongeza nguvu katika kusaidia wananchi kupata huduma ya matibabu ya saratani.