Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Tume ya Nguvu za Atomu Tanzania

"Mionzi kwa Matumizi Salama na Teknolojia ya Nyuklia kwa Maendeleo ya Taifa"
Nyumbani / Habari / ZANZIBAR KUJENGA TAASISI YA SARATANI

ZANZIBAR KUJENGA TAASISI YA SARATANI

ZANZIBAR KUJENGA TAASISI YA SARATANI

Published on February 13, 2026

Article cover image

Katibu Mkuu Wizara ya Afya Zanzibar, Dkt. Mngereza Mzee Miraji amesema Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar imejipanga kuanza ujenzi wa Taasisi ya Saratani Zanzibar mwaka huu ujenzi ambao utadumu kwa kipindi cha miaka miwili ili kusaidia wananchi kuondokana na changamoto ya kupata matibabu ya saratani nje ya Zanzibar jambo linalowagharimu muda pamoja na fedha nyingi.

Dkt. Miraji ameyasema hayo baada ya kupokea ugeni kutoka Wakala wa Kimataifa wa Nguvu za Atomu duniani (IAEA) ugeni ulioongozwa na Bwana Gashaw Gebeyehu Wolde, Kaimu Mkurugenzi wa Idara ya Ushirikiano wa Kiufundi kwa Afrika, pamoja na Bi. Azza Kashlan, Afisa wa Usimamizi wa Programu.

Kwa upande wake Kaimu Mkurugenzi wa Idara ya Ushirikiano wa Kiufundi kwa Afrika, Gashaw Gebeyehu Wolde amesema Wakala wa Kimataifa wa Nguvu za Atomu duniani (IAEA) upo tayari kuisaidia Zanzibar kupeleka wataalamu wa afya nje yan chi kupata mafunzo ili waje kutumika katika taasisi hiyo kutoa  huduma ya matibabu kwa wananchi.

Mkurugenzi Mkuu wa Tume ya Nguvu za Atomu Tanzania Prof. Najat Kassim Mohammed amesema ziara ya viongozi kutoka IAEA imelenga kutembelea miradi iliyopo katika sekta ya afya na kilimo ambayo inafadhiliwa na IAEA ili waweze kuona maendeleo ya miradi na namna inavyowasaidia wananchi.