Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Tume ya Nguvu za Atomu Tanzania

"Mionzi kwa Matumizi Salama na Teknolojia ya Nyuklia kwa Maendeleo ya Taifa"
Nyumbani / Habari / Tanzania Yaadhimisha Siku ya Kimataifa ya Wanawake na Wasichana katika Sayansi

Tanzania Yaadhimisha Siku ya Kimataifa ya Wanawake na Wasichana katika Sayansi

Tanzania Yaadhimisha Siku ya Kimataifa ya Wanawake na Wasichana katika Sayansi

Published on February 13, 2026

Article cover image

Dodoma, Februari 11, 2026 – Tanzania imeungana na mataifa mengine duniani kuadhimisha Siku ya Kimataifa ya Wanawake na Wasichana katika Sayansi, hafla imefanyika katika Ukumbi wa Jakaya Kikwete jijini Dodoma.

Maadhimisho hayo yalihudhuriwa na wadau mbalimbali wa elimu, sayansi na teknolojia, ambapo mgeni rasmi alikuwa Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia, Mhe. Prof. Adolf Mkenda. Akizungumza katika hafla hiyo, Prof. Mkenda alisisitiza umuhimu wa kuimarisha ushiriki wa wanawake na wasichana katika nyanja za sayansi na teknolojia, akibainisha kuwa mchango wao ni muhimu katika kufanikisha maendeleo endelevu ya taifa.

Katika tukio hilo, washiriki walipata fursa ya kutembelea banda la Tume ya Nguvu za Atomu Tanzania (TAEC) na kujionea shughuli pamoja na ubunifu unaotekelezwa na taasisi hiyo katika kukuza sayansi na teknolojia nchini.

Maadhimisho ya mwaka huu yalibeba kaulimbiu: “Muunganiko wa Akili mnembo na Sayansi Jamii, STEM na Fedha kuelekea Dira ya 2050: Kujenga Mustakabali Jumuishi kwa Wanawake na Wasichana.” Kaulimbiu hii inalenga kuhamasisha ushiriki mpana wa wanawake na wasichana katika masuala ya sayansi, teknolojia, uhandisi na hisabati (STEM), ili kuchangia katika kujenga jamii jumuishi na yenye maendeleo endelevu.