Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Tume ya Nguvu za Atomu Tanzania

"Mionzi kwa Matumizi Salama na Teknolojia ya Nyuklia kwa Maendeleo ya Taifa"
Nyumbani / Habari / Tanzania Yafanya Warsha ya Kikanda Kuhusu Mkataba wa Ulinzi wa vyanzo vya Nyuklia (CPPNM)

Tanzania Yafanya Warsha ya Kikanda Kuhusu Mkataba wa Ulinzi wa vyanzo vya Nyuklia (CPPNM)

Tanzania Yafanya Warsha ya Kikanda Kuhusu Mkataba wa Ulinzi wa vyanzo vya Nyuklia (CPPNM)

Published on June 23, 2025

Article cover image

Dar es Salaam, 23 Juni 2025 – Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kupitia Tume ya Nguvu za Atomu Tanzania (TAEC), leo imezindua rasmi warsha ya kikanda inayolenga kuhamasisha utekelezaji wa Mkataba wa Kimataifa wa Ulinzi wa vyanzo vya nyuklia (CPPNM) na marekebisho yake. Warsha hii inafanyika katika Hoteli ya Four Points by Sheraton, Dar es Salaam.

Warsha hii imewakutanisha washiriki 48 kutoka nchi mbalimbali za Afrika ambazo ni wanachama wa Shirika la Kimataifa la Nguvu za Atomiki (IAEA), shirika la Umoja wa Mataifa lenye makao yake makuu mjini Vienna, Austria.

Mgeni rasmi, Profesa Daniel Mushi, Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia, alizindua warsha hiyo kwa kusisitiza umuhimu wa kuimarisha usalama wa vyanzo vya nyuklia na ushirikiano baina ya nchi za Afrika. Alithibitisha kuwa serikali ya Tanzania imejizatiti kuhakikisha usalama wa vyanzo hivyo muhimu.

Mwenyekiti wa Bodi ya TAEC, Profesa Joseph Msambichaka, aliwakaribisha washiriki na kueleza jitihada zinazofanywa ndani ya ukanda na kimataifa katika kuimarisha ulinzi wa vyanzo vya nyuklia. Alisema Tanzania inajivunia kuwa kinara katika kuhamasisha nchi za Afrika kuridhia mkataba huu na marekebisho yake.

Mkurugenzi Mkuu wa TAEC, Profesa Najat Kassim Mohammed, alitoa shukrani kwa IAEA na wadau wote waliohusika katika kuandaa warsha hii. Alisisitiza umuhimu wa kushirikiana ili kuhakikisha vyanzo vya nyuklia vinatumika kwa njia salama na kwa matumizi ya amani pekee.