Warsha juu ya Majadiliano ya Pamoja ya Sheria Moja ya Udhibiti Katika Uchimbaji wa Madini ya Urani

Nov 19, 2019

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kupitia Tume ya Nguvu za Atomiki Tanzania (TAEC) kwa kushirikiana na Jumuiya ya Ulaya (EU)  inaendesha warsha ya kuboresha shughuli za kisheria na uhakiki ili kuboresha  uwezo uliopo katika kudhibiti madini ya urani. Warsha hii ya siku tatu ambayo imeanza tarehe 19 hadi  tarehe 21, Novemba 2019 katika makao makuu ya TAEC yaliyopo Njiro, Arusha

Lengo la warsha hii ni kujadili tathimini ya ripoti ya Sheria ya udhibiti na mahitaji na  ya leseni ya uchimbaji wa madini ya urani. Pia katika warsha hii muhitasari wa uwepo wa madini ya urani pamoja na utayari wa utoaji wa leseni ya uchimbaji wa madini ya urani katika siku zijazo pia utajadiliwa.

Mkurugenzi Mkuu wa TAEC, Profesa Lazaro Busagala akifungua warsha hiyo kwa niaba ya Mhe. Naibu Waziri wa Wizara ya Madini,  amesema majadiliano ya warsha yanalenga kuja  na sheria mpya itakayoweza kutumika katika uchimbaji wa madini ya Urani  pamoja na kumlinda mwananchi wa kawaida na madhara ya madini hayo.

“Kunahitajika udhibiti wa hali ya juu katika madini ya urani, hivyo sheria mpya itakapokamilika itaanza kutumika “alisema Prof.Lazaro .

Jumla ya washiriki 29 wanashiriki katika warsha  hii ambapo washiriki ishirini (20) ni kutoka TAEC na washiriki wengine tisa (9) ni kutoka taasisi nyingine ambazo zinahusika katika maswala ya madini ya urani kama vile, Wizara ya Madini, Wizara ya elimu, Sayansi na Teknolojia, Baraza la Taifa la Usimamizi wa Mazingira (NEMC), Wizara ya Maji, Wizara ya Maliasili, Ofisi ya Mwanasheria Mkuu na Tume ya Madini

Hifadhi za nyaraka