Kitengo cha Ukaguzi wa Ndani

Kuhusu Kitengo

Kitengo cha Ukaguzi wa Ndani:

Kitengo hiki kinawajibika  na shughuli za kupanga, kuratibu na kutekeleza shughuli zinazohusiana na ukaguzi wa mahesabu, uchambuzi na uhakiki wa shughuli za Tume kulingana na miongozo mbalimbali ya ukaguzi wa ndani; uhakiki wa mifumo kulingana na udhibiti wa vihatarishi; kuandaa taarifa za ukaguzi wa ndani na kuwasilisha kwa Mkurugenzi Mkuu, Kamati ya Ukaguzi na idara/vitengo husika vilivyokaguliwa; kufanya ukaguzi maalum; kufuatilia utekelezaji wa ushauri wa taarifa za ukaguzi; kuandaa mpango kazi wa mwaka wa ukaguzi wa ndani pamoja na kushauri kuhusu matumizi bora ya rasilimali za Tume.

 Wafanyakazi:

Kitengo cha Ukaguzi wa ndani kina wafanyakazi watatu ambao ni:

  1. Innocent E. Mapendo             Mkuu wa Kitengo, Ukaguzi wa Ndani
  2. Janeth A. Lema             Ofisa Mkuu, Ukaguzi wa Ndani
  3. Mary A. Riwa                                     Ofisa, Ukaguzi wa Ndani

 Mawasiliano:

Kwa mawasiliano juu ya kitengo cha ukaguzi wa ndani, wasiliana kwa barua pepe: innocent.mapendo@taec.go.tz

 

Vitendea Kazi:        

Vitendea kazi vinavyotumika katika ukaguzi wa ndani ya Tume ni;

  • Mpango kazi wa Tume, 2023/24 – 2025/26.
  • Mwongozo wa Ukaguzi wa ndani wa Tume.
  • Mkataba wa huduma kwa Mteja.
  • Sera na Mwongozo wa Taratibu za Kiuhasibu wa Tume.
  • Muundo wa Utumishi wa Tume.
  • Kanuni za Utumishi za Tume.
  • TAEC ‘’Various Procedures in Radiation control and Nuclear Technology Directorates’’.
  • Sheria ya fedha Na. 6 ya mwaka 2001 na kanuni zake za mwaka 2005’’.
  • Sheria ya Manunuzi ya mwaka 2016 na kanuni zake.
  • Sheria ya Nguvu za Atomiki Na. 7 ya mwaka 2003 na kanuni zake .
  • Viwango vya kimataifa vya ukaguzi.
  • Viwango vya kimataifa vya kiuhasibu kwenye Sekta za umma.
  • Nyaraka za Serikali.
  • ‘’International Professional Practice Framework’’ (IPPF)
  • Kanuni za maadili.
  • Mwongozo wa ukaguzi wa ndani wa Sekta ya Umma.
  • Mwongozo wa Kamati ya ukaguzi wa Sekta ya Umma.

 Maelezo ya Kanuni na Miongozo:

  1. ‘’International Professional Practice Framework’’ (IPPF) – Ni mfumo wa dhana ambao unatoa mwongozo wa kimamlaka katika taaluma ya ukaguzi uliobuniwa na Taasisi ya Wakaguzi wa Ndani. Miongozo ya IPPF inahusisha Maana ya Ukaguzi wa Ndani, Miiko ya Ukaguzi wa Ndani na Kanuni za Kimataifa Katika Ukaguzi wa Ndani.
  2. Kanuni za Kimataifa za Ukaguzi (ISA) – Ni taratibu za kimataifa za kitaaluma kuhusu ukaguzi wa taarifa za fedha. Taratibu hizi zinatolewa na waratibu wa uandaaji kanuni hizi ambao ni IFAC kupitia IAASB.
  3. Kanuni za Kimataifa za Mahesabu Katika Sekta ya Umma (IPSAS) – Ni taratibu za kimataifa za uandaaji taarifa za mahesabu katika sekta ya umma pamoja na mashirika yake.
  4. Kanuni za Kimataifa za Mahesabu (IAS) – Ni taratibu za awali za kimataifa za uandaaji mahesabu zilizotolewa na IASB, taasisi ya kutunga kanuni za mahesabu iliyopo London. Kanuni hizi zilibadilishwa mwaka 2001 kuwa Kanuni za Kimataifa za Uandaaji Taarifa za Mahesabu (IFRS).
  5. Kanuni za Maadili – Ni miiko ya kimaadili na kitaaluma inayotoa misingi inayowasaidia wanataaluma kufanya kazi kwa uaminifu na ustadi. Kanuni hizi huonesha dira na miiko ya biashara au taasisi, namna wanataaluma wanavyotakiwa kutatuwa changamoto, misingi ya kimaadili kulingana na vigezo vya kitaasisi pamoja na taratibu zinazombana mwanataaluma katika kutenda majukumu.
  6. Miongozo ya Kiserikali – Ni maandiko ya kisera ambayo yanatoa taarifa, miongozo, kanuni na muhtasari kuhusu serikali au masuala ya kiutaratibu.

Habari na matukio ya Kitengo

Hakuna Matokeo Iliyopatikana

Ukurasa uliouomba haukuweza kupatikana. Jaribu kusafisha utafutaji wako, au tumia urambazaji hapo juu ili kupata chapisho.

Hifadhi za nyaraka