Mahusiano na Mawasiliano

Kuhusu Kitengo

   Kazi ya kitengo hiki ni kumshauri Mkurugenzi Mkuu juu ya mambo yanayohusiana na mawasiliano, utoaji wa taarifa na uelimishaji kwa  umma juu ya  majukumu yanayotekelezwa na  Tume kisheria ili kuimarisha mahusiano ya ndani na nje ya Tume kuanzia ngazi ya kitaifa, kikanda na kimataifa.

Kazi za Kitengo cha Mawasiliano
Kutoa ushauri wa kitaalamu na huduma kwa Taasisi katika Nyanja za upashaji taarifa, mawasiliano na elimu kwa umma
Kitengo hiki kinafanya kazi zifuatazo:

 • Kutayarisha na kusambaza taarifa mbalimbali kupitia vipeperushi, taarifa  kupitia makala mbalimbali kwenye vyombo vya habari kwa lengo la kuhamasisha na kuelimisha jamii juu ya majukumu ya Tume yanayohusisha matumizi salama ya teknolojia ya nyuklia na udhibiti wake.
 • Kuandaa mikutano na waandishi wa habari na kuujulisha umma juu ya kazi mbalimbali za Tume.
 • Kuandaa mahojiano ya Televisheni na Redio,
 • Kuandaa jumbe mbalimbali za video na Redio zenye lengo la utoaji elimu kwa jamii juu ya kazi za Tume.;
 • Kufanya maandalizi na usaidizi kwenye ushiriki mbalimbali kama vile mikutano, semina warsha zinazofanywa na Tume;
 • Kushiriki kwenye utoaji wa elimu nje ya ofisi kama vile maonesho mbalimbali ya matukio, mafunzo nk;
 • Kushiriki kwenye midahalo mbalimbali ya wananchi, kwenye vyombo vya habari, juu ya masuala mbalimbali ya Tume na yanayohitaji kuyatolea ufafanuzi
 • Kuhamasisha kufuatwa kwa taratibu na sheria za Tume katika kazi zake kuu za udhibiti wa matumizi salama ya mionzi nchini
 • Kuandaa taarifa mbalimbali za Tume kwa ajili ya vyombo vya habari, warsha na mikutano;
 • Kuandaa na kusambaza taarifa mbali mbali juu ya kazi za Tume kwenye mitandao ya kijamii.
 • Kuweka taarifa  mbalimbali kwenye Tovuti ya Tume
 • Kushauri Idara, Vitengo na Skesheni ndani ya Tume namna ya kuandaa taarifa zao kwa ajili ya kuwekwa kwenye tovuti.

Watendaji
Kitengo cha Uhusiano kina watendaji wawili (2)

 1.  Peter G. Ngamilo- Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano
 2. Angella Msangi- Afisa Uhusiano

Mawasiliano;
           Barua Pepe: peter.ngamilo@taec.go.tz
           Namba ya Simu: +255 755 496 515

Habari na matukio ya Kitengo

Hakuna Matokeo Iliyopatikana

Ukurasa uliouomba haukuweza kupatikana. Jaribu kusafisha utafutaji wako, au tumia urambazaji hapo juu ili kupata chapisho.

Hifadhi za nyaraka