Kitengo cha Tehama na Takwimu
Kuhusu Kitengo
Kitengo cha Teknolojia ya Habari na Mawasiliano na takwimu kina lengo la kutoa huduma za kitaalamu juu ya matumizi ya teknolojia ya habari na mawasiliano pamoja na takwimu kwa Tume.
Majukumu ya Kitengo cha cha TEHAMA na TAKWIMU
- Kutayarisha mpango Mkakati wa kuhusu teknolojia ya habari na mawasiliano, Miongozo na taratibu kwa kuzingatia Sera ya Taifa ya Teknolojia ya Habari na Mawasiliano.
- Kuishauri Menejimenti juu ya masuala yanayohusiana na sera, miongozo na taratibu zinazohusiana na takwimu.
- Kutumia teknolojia ya habari na mawasiliano kwenye kushughulikia takwimu na taarifa, kutunza, kuzipitisha hatua mbalimbali, kuzichambua, kuziwasilisha, kuzisambaza na kuzihifadhi.
- Kuishauri Menejimenti juu ya masuala yanayohusiana na sera zinazohusiana na teknolojia ya habari na mawasiliano na utekelezaji wa dhana ya serikali mtandao.
- Kusimamia maendeleo ya teknolojia ya habari na mawasiliano na utekelezaji wake.
- Kuratibu na kuendeleza viwango vya teknolojia ya habari na mawasiliano kwa ajili ya “software na hardware” kwa matumizi ya Tume.
- Kuziwezesha Kurugenzi, idara, vitengo na seksheni kuendeleza na kutekeleza mipango/miradi ya teknolojia ya habari na mawasiliano.
- Kuratibu utekelezaji wa usanifu na kutunza/kuiendeleza matumizi yanayohusiana na Tovuti na utunzaji wa kumbukumbu kwa ajili ya Tume.
- Kutathimini, kuboresha na kusimamia teknolojia ya habari na mawasiliano na usimamizi wa mifumo ya taarifa/habari iliyosimikwa/iliyowekwa kwenye Tume.
- Kufanya tathimini ya mahitaji ya mafunzo juu ya usimamizi wa mifumo ya taarifa na teknolojia ya habari na mawasiliano na kuandaa mpango wa kujenga uwezo
- Kufanya tathimini ya hatari/hasara zinazohusiana na miundombinu ya teknolojia ya habari na mawasiliano na mfumo wa usimamizi wa taarifa na namna ya kuthibiti.
- Kuendeleza na kutunza Tovuti ya Tume
- Usimamizi wa Mifumo ya Kompyuta (System Administration)
- Usimamizi wa Mtandao wa Kompyuta pamoja na vifaa vyake (Network and Hardware Adminstration).
- Usimamizi wa kanzi data (Database Administration)
- Usimamizi wa tovuti na barua pepe (website administration & emails).
- Kutekeleza sera ya TEHAMA na Serikali Mtandao.
- Kuandaa mahitaji katika Ununuzi wa vifaa vya TEHAMA.
- Kuweka usalama wa hifadhi data.
- Kutoa huduma za hifadhi data kwa watumiaji.
- Kusimamia maboresho ya programu za kompyuta kwa wakati.
- Kusakinisha, kusanidi na kuboresha programu za kuzuia virusi vya kompyuta. (Install, configure and update antivirus software).
- Kuelimisha watumiaji masuala mbalimbali yanayohusu usalama, hatari na udhaifu katika mifumo ya TEHAMA.
- Kukagua mifumo ya TEHAMA mara kwa mara.
- Kuweka viwango vya usalama na udhibiti katika mifumo ya TEHAMA kwa watumiaji.
- Kusanifu, kusakinisha na kusanidi miundombinu ya ndani na nje ya mtandao wa kompyuta (Design, install and configure LAN and WAN infrastructure).
- Kufanya majaribio ya vifaa vya mtandao wa kompyuta.
- Kushauri kitaalam katika manunuzi ya vifaa bora na vya kudumu vinavyohusu TEHAMA.
- Kutengeneza vifaa vyote vya TEHAMA vinapoharibika au kutofanyakazi iliyokusudiwa kwa kupitia kwa fundi sanifu wa Kompyuta.
- Kusimamia mifumo ya kompyuta hasa mifumo ya Mapato na Mashine za Kukusanyia Mapato (Point Of Sales – POS).
- Kuboresha miundombinu ya TEHAMA.
- Kuimarisha ufanisi wa ufanyaji kazi wa kompyuta kwa kufanya matengenezo ya mara kwa mara.
- Kuwaelekeza watumiaji namna sahihi ya kutumia kompyuta ili ziweze kudumu kwa muda mrefu
- Kuboresha upatikanaji wa taarifa sahihi na haraka zenye ufanisi kwa kutumia tovuti na barua pepe za serikali kwa kushirikiana na Wakuu wa Idara/Vitengo mbalimbali.
Habari na matukio ya Kitengo
Mwongozo wa Taarifa kwenye Tovuti
Sera na Miongozo Kuhusu TEHAMA
1. SERA YA TEHAMA Madhumuni ya sera hii ni kuhakikisha kuwa matumizi ya TEHAMA yanachangia katika utendaji bora na kuongeza tija, kukuza utafiti, usalama wa matumizi ya teknolojia ya nyuklia kwa ajili ya maendeleo ya wananchi na Taifa kwa ujumla. Teknolojia ya Habari...
Kuunganisha Mfumo wa Kielektroniki wa Dirisha moja na Mfumo wa Kutoa Vibali vya Mionzi
SERIKALI kupitia Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA), imeendelea na mikakati yake ya kuhakikisha inaweka mazingira mazuri kwa wafanyabiashara wote wa ndani na nje ili waweze kufanya biashara bila usumbufu na kulipa kodi stahiki kwa hiari kwa mujibu wa sheria.Moja ya...