Mafunzo ya Usimamizi wa Usalama wa Mionzi kwenye Vifaa Vitunavyotumia Mionzi

Feb 20, 2020

Tume ya Nguvu za Atomiki Tanzania (TAEC) inaendesha  mafunzo ya siku tano juu ya usimamizi wa usalama wa mionzi kwa wafanyakazi wanaotumia  vifaa vitumiavyo mionzi migodini, viwandani na kwa watengenezaji wa vifaa vya mionzi vya hospitalini. Mafunzo haya yaliyoanza jumatatu katika Makao Makuu ya TAEC yanatarajiwa kufungwa rasmi siku ya ijumaa tarehe 21 Februari, 2020

Lengo kuu la mafunzo haya ni kutoa elimu kuhusiana na mionzi, matumizi salama ya mionzi, madhara yanayoweza kujitokeza kutokana na mionzi, Sheria inayosimamia udhibiti wa matumizi salama ya mionzi, namna bora ya kujikinga dhidi ya madhara ya mionzi kwa kuzingatia kanuni za ulinzi wa mionzi (Radiation Protection Principals) katika kuhakikisha usalama wa watumiaji na watengenezaji wa mashine za Midaki (X-Ray Baggage Scanner).

Akifungua rasmi mafunzo hayo leo, Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa TAEC Dkt. Justine Ngaile amesema mafunzo haya yatawawezesha washiriki kupata elimu juu ya matumizi salama ya vyanzo vya mionzi ili kujikinga na madhara yanayoweza kusababishwa na mionzi katika maeneo yao ya kazi.

Jumla ya idadi ya washiriki katika mafunzo haya ni kumi na sita (16) kutoka mgodi wa Bulyahulu, Kampuni ya soda ya Coca-Cola Kwanza, Serengeti Breweries, Watengenezaji wa vifaa vya mionzi (Repair and Maintenance of Nuclear Equipments) , Hospitali ya Bugando, Oceanic Pacific na Archelis

Hifadhi za nyaraka