Mkurugenzi Mkuu wa Tume Ya nguvu za Atomiki Tanzania Prof. S.P.Busagala amefanya mkutano na Wafanya Biashara kanda ya Ziwa

May 17, 2019

Mkurugenzi Mkuu wa  Tume ya Nguvu za Atomiki Tanzania (TAEC )Prof. Lazaro Busagala aliyekaa katikati katika picha ya pamoja na Wafanyabiashara wa kanda ya Ziwa mara tu baada ya kuwasilisha mada katika mkutano uliofanyika kati ya Tume ya Atomiki Tanzania(TAEC )na wafanyabiashara hao wa bidhaa za Samaki na aina zingine mbalimbali za vyakula wa kanda ya Ziwa

Katika mkutano huo Prof. Busagala aliwasilisha mada juu ya majukumu ya Tume ya Nguvu za Atomiki Tanzania  kisheria   ili kuongeza Uelewa na kujadiliana hatua  mbalimbali ambazo zitaisaidia Tume hiyo kuboresha mazingira ya ufanyaji biashara kwa wafanyabiashara wa  Mkoa wa Mwanza na wafanyabiashara wote wanaolizunguka ziwa Victoria
Hii ikiwa ni pamoja na kuangalia mapungufu mbalimbali na hatimaye kuyachukulia hatua ili kuweka ustawi mzuri kati ya wafanayabiashara hawa na Tume ya Nguvu za Atomiki Tanzania ( TAEC) ambayo ndio mamlaka pekee yenye dhamana ya Udhibiti wa mionzi na uhamasishaji Salama wa matumizi ya teknolojia ya Nyuklia  hapa nchini.

Katika mkutano huu Prof. Busagala amewaeleza wafanyabiashara hao kuwa athari za mionzi zinaweza kuleta madhara makubwa endapo kutakuwa na ukiukwaji wa kisheria

Pia Prof. Busagala alisisitiza kuwa umakini na ushirikiano mkubwa unahitajika ili kuendelea kudhibiti na kuna ulazima mkubwa wa kupima bidhaa hizo ili kukidhi matakwa ya sheria ya Nguvu za Atomiki (Atomic Act No 7) na Sheria za Kimataifa kwani kwa kutokufanya hivyo kutakuwa na ukiukwaji sheria iliyopo  ya udhibiti wa mionzi ili kutosababisha madhara yanayoweza kusababishwa na vimelea vya mionzi kwa wananchi na mazingira

Hifadhi za nyaraka